Are you an artist? Make the most of your lyrics with Musixmatch Pro!
Verified by Curator
3 contributions
about 2 years ago
Translations

Lyrics of Muongo by Rose Muhando

Kweli mizani ya hadaa ni chukizo baya
Ni uangamivu ulio karibu,
Mtu mjinga huamini kila aambiwalo bali mwenye hekima hufikiri sana,
Apendaye mafundisho hupenda maarifa bali achukiaye ni kama mnyama,
Mtu mjinga huamini kila aambiwalo
Kijapo kiburi huja aibu,
Yuko wapi rafiki yako mlopendana siku ya kwanza mlipokutana, yuko wapi?
Aliyesema anakupenda mpaka kifo kiwatenge leo yuko wapi rafiki yako?
Alikupa ahadi nyingi na viapo tele, leo yuko wapi rafiki yako?
Mbona amekukimbia umebaki pekee yako unahuzunika pole we!
Alisema anachanganyikiwa, nisipoiona sura yako leo yuko wapi rafiki yako?
Alikuja na vicheko na furaha tele, leo yuko wapi rafiki yako?
Mbona unateketea ah, unaangamia amekwenda zake rafiki yako!
Tumemwona mtaa wa pili
Anakwenda zake amekusaliti rafiki yako!
Wenye dhambi wakikushawishi mwanangu kataa usiwafuate utaangamia,
Watakuja na maneno mazuri tamu kama asali usiwasikize ni walaghai,
Watakuja wenye sura zuri tena mvuto wa ajabu usiwatazame ni walaghai,
Hata wawe na shape nzuri, zuri kama nini, usiwatazame utaangamia!
Kucheza na marafiki wabaya epuka mwanangu ni sawa na kushika sikio la simba!
Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo ′tavunjika ghafla hapati dawa
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Rafiki yako,
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Anakulaghai
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Rafiki tapeli
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Rafiki wabaya
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Rafiki yako,
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Japo anacheka nawe,
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Japo anatembea nawe,
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
_Anawinda roho yako,
MUONGO RAFIKI YAKO MUONGO
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU!
_Rafiki mwema,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Pendo lake la milele,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Yeye huponya magonjwa,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Jina lake ni faraja
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Wamwendeao wanapona
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Ukimwita anaitika,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Ukimwita anaitika,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
_Sikio lake si zito,
NI YESU RAFIKI MWEMA NI YESU
Writer(s): Rose Muhando

Contribute

To-do

Structure Tag
Identify the song's sections

Completed

Lyrics
Verified by Curator
Performers Tag
Identify who's singing what

Credits

This song has no credits yet

Contributions

Last edit about 2 years ago
Are you an artist? Distribute your lyrics!
Take full control of your lyrics. Curate, sync, and distribute your lyrics on Spotify, Apple Music, and more.
Explore Musixmatch Pro